Habari za Mastaa

Kundi maarufu la muziki; ‘One Direction’ kutengana…?! Ukweli huu hapa.

on

One Direction (left to right) Liam Payne, Niall Horan, Louis Tomlinson and Harry Styles backstage at the Capital FM Summertime Ball held at Wembley Stadium, London.

Niall Horan, Liam Payne, Harry Styles na Louis Tomlinson pamoja wanaunda kundi maarfu la muziki ‘One Direction’. One Direction ni kundi kutoka Uingereza ambao kwa pamoja wamekuwa wakifanya muziki kwa miaka 5 sasa.

Awali kundi hili lilikuwa la watu watano, Zayn Malik alijitoa kwenye kundi hili mwanzo wa mwaka huu na hivyo kubakia 4… headlines za One Direction zilikuwa nyingi sana baada ya tetesi nyingi kusambaa kuwa kundi hili linatengana baada ya miaka 5 ya kazi.

one-direction

One Direction kabla ya Zayn Malik  (wa pili kushoto) hajajitoa kwenye kundi hili.

Msemaji wa kundi la One Direction ameamua kuweka wazi ukweli wa tetesi zote tunazosikia akiwa kwenye moja ya interviews msemaji huyo alisikika akisema…

>>> ” Ndio wamekuwa pamoja kwa miaka 5, safari ambayo imekuwa ndefu, ngumu na yenye matumaini… lakini ukweli ni kwamba kundi hili halitengani kama wengi wanavyosema bali wamekubaliana kuchukua mapumziko ya mwaka mmoja ili kila mtu awe huru kufanya project zake binafsi… ila kwa sasa tutegemee show yao ya mwisho itakayokuwa mwishoni mwa mwezi October.”<<< nuku ya msemaji wa One Direction.

one direction2

 One Direction wako kwenye chati na wimbo wao mpya ‘Drag Me Down’, walioutoa tarehe 20 August na imepita wiki moja tu toka video yao iachiwe, lakini ukienda kwenye ukurasa wao wa YouTube utagundua kuwa ndani ya wiki moja tu video hio imepata watazamaji million 27,700,970!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Soma na hizi

Tupia Comments