Inaelezwa kuwa Tanzania kuna Ongezeko la Wagonjwa wa Saratani wapatao 50,000 na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na ongezeko la asilimia 50 ya wagonjwa wapya wa saratani.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto, Dk. Dorothy Gwajima wakati wa uzinduzi wa idara ya magonjwa ya saratani, huduma za patholojia na makataba wa mteja kwenye Hospitali ya Benjamini Mkapa.