Michezo

Ronaldo katimiza siku 38 bila kufunga goli Bernabeu Madrid ikiichapa Bilbao

on

Najua Jumapili ya October 23 2016 kulikuwa na michezo mingi ya Ligi Kuu mbalimbali barani Ulaya, mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao ulikuwa ni moja kati ya michezo ya kuvutia iliyochezwa usiku wa Jumapili ya October 23.

39a5973800000578-3865128-image-a-184_1477255498513

Real Madrid walishuka dimbani kuwakaribisha Athletic Bilbao kucheza mchezo wao wa 9 wa Ligi Kuu Hispania, ikiwa nyota wao Cristiano Ronaldo aliingia katika mchezo huo akiwa na kumbukumbu ya mara ya mwisho kufunga goli katika uwanja wa Santiago Bernabeu September 14 2016, sawa na siku 38 bila goli na hicho ndio kipindi chake kirefu kuwahi kukaa bila kufunga goli Bernabeu toka amejiunga na timu hiyo.

39a53ae500000578-3865128-image-a-134_1477253041040

Real Madrid walifanikiwa kuzibakisha point zote tatu nyumbani kwa kuifunga Athletic Bilbao goli 2-1, Real Madrid walipata goli la kwanza dakika ya 7 kupitia kwa Karim Benzema aliyetumia vyema assist ya Isco ila Bilbao wakasawazisha dakika ya 27 kupitia kwa Sabin Merino, mchezo ulizidi kuwa mgumu Real Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 83 Alvaro Morata alifunga goli la ushindi.

liga

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments