Duniani

Magari ya kifahari ya jeshi la Polisi Dubai, unakamatwa na kosa barabarani unasahau faini ukilishangaa gari

on

Dubai ni moja ya sehemu ukienda kwa mara ya kwanza utajikuta unashangaa tu tena kama wewe ni mpenzi wa magari makali na maisha mengine ya kifahari ndio kabisa maana kuanzia watu binafsi mpaka Jeshi la Polisi wanayo magari ya kifahari kama Ferrari, Bugatti na Lamborghini ambayo wengi wetu tumezoea kuyaona kwenye video za mastaa wa dunia kama kina Nicki Minaj, Chris Brown na wengine.

Dubai ni moja ya sehemu chache duniani zenye usalama wa hali ya juu, mtaani hata iwe saa kumi au tisa usiku hakuna uhalifu na ninakumbuka mwaka 2014 nilifanya mahojiano na mwenyeji wa Dubai kwa zaidi ya miaka 20 akasema vitu kama wizi wa ukabaji au Majambazi hakuwahi kuvisikia, ishu alizowahi kuzisikia ni kama za visa vya mapenzi tu watu kupigana au kumletea mtu fujo sababu kakuchukulia mpenzi wako.

Kwenye hizi video hapa chini kuna Makala inayoonyesha Polisi wa Dubai wanavyofanya kazi na magari ya kifahari ya jeshi hilo ambayo yanaspidi kubwa kuliko magari ya kawaida lakini pia teknolojia waliyonayo kwenye kufatilia ishu za kiusalama.

HIZO HAPO JUU NI ZA POLISI, ZA RAIA MTAANI NI HIZI HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments