Jeshi la Polisi nchini limefanya operesheni maalum ijulikanayo kwa jina ‘Operesheni Wami’ ikishirikisha Mikoa minne ya Tanga, Pwani, Morogoro na Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kwa muda wa siku 45, hii ni kutokana na ongezeko la matukio ya uhalifu ikiwemo wizi wa magari na pikipiki, ujangili na unyang’anyi wa kutumia silaha na matukio mengine.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi nchini Mihayo Msikhela ameelezea mafanikio ya operesheni hiyo na kusema wamekamata malighafi ya kutengeneza Pesa bandia, magari manne na pikipiki saba, silaha, ng’ombe 132, mbuzi 27, nyama ya nyumbu (nyara) kilo 7, dawa za kulevya, gongo n.k
Watuhumiwa waliokamatwa kwenye operesheni hiyo ni 262 na kati yao 195 waliohojiwa na kufikishwa Mahakamani.