Michezo

Kingine kilichonifikia kuhusu hatma ya mwanariadha Oscar Pistorius…

on

Maisha ya mwanariadha maarufu Oscar Pistorius gerezani yameendelea kubaki njiapanda baada ya wasimamizi wa kesi hiyo kushindwa kufikia muafaka wa kumuondoa gerezani.

Jana bodi inayosimamia kesi yake ilikutana kwa lengo la kumtoa mwanariadha huyo lakini walishindwa kuafikiana.

Wakili wake Brian Webber ameiambia AFP kuwa rufaa yake ya kuachiwa imerudishwa tena kwa bodi ya usimamizi wa kesi hadi hapo itakaposomwa tena.

Mwanariadha huyo amefungwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Oscar pamoja na wakili wake na ndugu zake wamekuwa wakijaribu kila liwezekanalo ili aweze kuwa huru lakini mpaka sasa bado haijawezekana.

Mwezi August Oscar alikuwa aruhusiwe kutoka jela lakini ikashindikana baada ya mwendesha mashtaka Michael Masutha kukataa dakika za mwisho

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments