Duniani

Kesi ya mauaji inamrudisha tena Oscar Pistorius Mahakamani South Africa…

on

Kitu cha mwisho kimegusa headlines kuhusu mwanariadha wa South Africa, Oscar Pistorius ilikuwa ishu ya kuachiwa kutoka gerezani na kutumikia kifungo akiwa nyumbani kwa mjomba wake, Pretoria.

Mambo huenda yakabadilika, mashtaka ya Oscar Pistorius yamerudishwa tena Mahakamani ambapo safari hii kesi inabadilishwa na waendesha mashtaka wametaka hukumu yake iwe ya mauaji ya kukusudia na sio ya mauaji ya bahati mbaya.

Oscar Pistorius tayari amekaa jela mwaka mmoja katika hukumu ya miaka mitano aliyopewa kabla ya kuhamishiwa kuendelea na hukumu ya kifungo cha nyumbani ambacho anatumikia nyumbani kwa mjomba wake, Pretoria.

Nyumba ya mjomba wa Pistorius.

Nyumba ya mjomba wa Pistorius.

Kwa mashtaka mapya yanayomkabili huenda kifungo chake kikafikia mpaka miaka 15 jela badala ya ile mitano aliyohukumiwa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments