Kama utakuwa unakumbuka siku kadhaa zilizopita alianza Prezzo kutangaza nia ya kuingia kwenye siasa kwa kupitia kura za wananchi kwenye nafasi ya ubunge katika jimbo la Kibra.
Taarifa hiyo ikapokelewa kwa mikono miwili na wakenya huku wengi wakimlingalisha na msanii mwenzake Jaguar ambae yeye kwasasa ni mbunge wa jimbo la Starehe.
Sasa Headlines zimehamia kwa msanii mwingine Rapper Octopizzo ambae hivi karibu alifanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto, Willy Tuva na kufunguka nia yake ya kugombea nafasi ya Urais mwaka 2022.