Michezo

Kamera za barabarani zikamnasa Mourinho akiwa spidi, Ishu ikafika mahakamani!!

on

MOOO

Nchi za wenzetu sheria za barabarani zimekua zikizingatiwa sana na imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na tatizo la ajali.

Kwa mfano ukipita kwenye taa wakati hazijaruhusu hata kama hakuna magari lazima utakamatwa na kuchukuliwa hatua.

Kuna kesi ambayo inamkabili kocha wa Chelsea, Jose Mourinho baada ya Mahakama kumfungia kuendesha gari kwa miezi sita baada ya kuendesha kwa kasi katika eneo ambalo haliruhusiwi.

Mourinho alifanya kosa hilo September mwaka jana na kunaswa na kamera akiendesha spidi 60 eneo alilotakiwa kuendesha spidi 50

Katika hukumu iliyotolewa Mahakama ya Staines jana, kocha huyo ametakiwa pia kulipa faini ya Pound 910 kwa kosa hilo la kuendesha gari kwa spidi 10 zaidi ya kiwango kinachotakiwa.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments