fB insta twitter

Alichokiandika Mwanasheria Alberto Msando kuhusu Msanii Harmorapa

on

Siku chache baada ya msanii Harmorapa kupata Ubalozi wa kinywaji kinachoitwa cider ‘swala’, Mwanasheria maarufu Alberto Msando ambaye amekuwa akizishughulikia kesi za watu maarufu kama Wema Sepetu na wengineo, ametoa pongezi kwa msanii huyo.

Msando alitoa pongezi hizo kwa Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram akimpongeza kwa hatua aliyopiga na kujitahidi kutengeneza umaarufu ambao wengi wameshindwa. 

Alberto Msando ameyaandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram…>>>I really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi hawawezi.

Wengi wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu. Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider ‘swala’. Its a big step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby ????.;- Msando

Kisa tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama wengine. #TheDon#HarmoMbio #HarmoBastola#KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa ??#NusuUsoNusuPua;-Msando

VIDEO: Harmorapa afunguka kwanini alikimbia baada ya kuona Nape katolewa Bastola

VIDEO: Mkudesimba na Stan Bakora Ibadani kwa Askofu Gwajima leo

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments