Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla Elon Musk aliwaacha mashabiki zake na watumiaji wa mtandao wa X namna ambavyo ameamua kuisherehekea Krismasi siku ya Alhamisi, akishiriki picha ambayo alikuwa amevaa kama Santa Claus.
Picha hiyo, iliyotumwa kwenye mtandao wake wa kijamii wa X, ilimuonyesha Bw Musk akiwa amevalia ndevu za Santa, mavazi ya rangi nyekundu na nyeupe, na amesimama na mikono yake kiunoni mbele ya mti mkubwa wa Krismasi.
“Ozempic Santa,” tajiri wa teknolojia aliandika kama nukuu.
Alilinganisha sura yake na mhusika wa filamu, akisema, “Kama Cocaine bear, lakini ni Santa Ozempic!”
Katika chapisho la pili, Bw Musk alishiriki tukio – picha yake ya utotoni akiwa amevalia kama Santa, akiwa ameshikilia begi jeupe na amesimama kwenye barabarani pembeni ya miti. Akilinganisha picha hizo mbili, aliandika, “Jinsi ilianza dhidi ya jinsi inavyoendelea.”