Michezo

Ozil kajitolea kumlipa mshahara Jerry Quy

on

Mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil ametangaza kuwa atajitolea kumlipa mshahara Mascot Jerry Quy ambaye alikuwa sehemu ya wafanyakazi wa Arsenal waliopunguzwa sababu ya uchumi kuyumba.

Ozil amesema Jerry Quy arejee kazini atamlipa mshahara kwa kipindi chote ambacho Ozil ataendelea kuitumikia Arsenal, Jerry Quy amefanya kazi hiyo Arsenal kwa miaka 27 sasa.

Baada ya mlipuko wa janga la Corona, vilabu vingi Ulaya vimeshindwa kulipa mshahara baadhi ya watumishi wake na kuamua kuwapunguza wakati wengine kuamua kuwakata mishahara.

Soma na hizi

Tupia Comments