Michezo

Fahamu siri ya uhusiano ya Ozil na kipa Manuel Neuer

on

Ozil_neu-scaled Najua namna Mesut Ozil anavyopiga penati. Nilijua angesubiri kwa muda kabla ya kuamua upande upi apige.” – Manuel Neuer akizungumza kuhusu kuokoa penati ya Mesut Ozil.

Mesut Ozil na Manuel Neuer wamekuwa wakicheza pamoja katika timu ya taifa ya Ujerumani kwa muda mrefu, pia walicheza pamoja katika timu ya umri chini ya miaka 21.

Pia leo hii imegundulika kwamba urafiki wa Mesut Ozil na Neur ulianza tangu walipokuwa wakisoma shule utotoni kama inavyoonesha hii picha hapo chini.

Bg3xDQVIcAAgKcl

Wote Mesut Ozil na Manuel Neuer walisoma shule ya Gesamtschule Berger Feld ambayo ipo karibu na uwanja wa klabu ya Schalke Veltins Arena.

Ni moja ya shule za secondary kubwa kabisa nchini na mara nyingi amekuwa akisomesha wachezaji ambao mbeleni huchezea klabu ya  Schalke. Ozil na Neuer wote walicheza pamoja pia katika klabu ya Schalke.

 

Tupia Comments