Watoto saba wa Rapper Sean Combs maarufu Diddy ambaye November 4 2024 ametimiza umri wa miaka 55, wameungana saa kadhaa zilizopita kuwasiliana kwa simu na kumtakia Baba yao heri ya siku ya kuzaliwa.
Diddy ambaye alizaliwa November 4 1969 Harlem, New York, amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani akisubiri hatma yake kuhusu kesi anazokabiliwa nazo.
Katika video iliyowekwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, Watoto wake wote saba walionekana kushiriki kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa kitendo ambacho kilimfurahisha Diddy na kuandika katika Instagram yake kuwa kitendo hicho kimeifanya siku yake kuwa bora “This made my day”.
“Ninawapenda nyote, nawapenda sana, siwezi kusubiri kuwaona… najivunia nyinyi nyote” asanteni nyote kwa kuwa imara na kuwa upande wangu, nawapenda sana…. ninayo familia bora duniani” alisikika Diddy katika maongezi hayo ya simu.
P Diddy amekuwa kizuizini tangu Septemba 17, 2024, baada ya kukana mashtaka ya kulazimisha wanawake kushiriki matukio ya kingono wakiwa wamelewa, pamoja na mashtaka mengine ya ulanguzi wa wanawake wanaojiuza na njama za ulaghai.
Mawakili wake wameomba dhamana ya dola milioni 50 ili awekwe chini ya ulinzi wa kifaa cha GPS akiwa nyumbani kwake Florida, lakini ombi hilo limekataliwa hadi sasa.
P Diddy alianzisha lebo ya Bad Boy Records mwaka 1993 na ni mmoja wa mabosi wakubwa kwenye tasnia ya muziki wa Hip Hop.