Moja ya habari kubwa iliyosambaa kwa kasi wikiendi hii kwenye ulimwengu wa ENT ni pamoja na Rapa Sean Combs al maarufu kama P. Diddy na Ex wake Cassandra Ventura wamefikia suluhu baada ya kesi iliyowasilishwa na mwanamke huyo akimtuhumu Diddy kwa ubakaji na unyanyasaji kipindi chote cha mahusiano yao yaliyoanza miaka 20 iliyopita.
Kupitia mwanasheria wake Cassie alisema “Nimeamua kutatua suala hili kwa amani kwa masharti ya kwamba nitakuwa na kiwango flani cha udhibiti, akiongeza kwa kusema “Ningependa kuishukuru familia yangu, mashabiki na wanasheria kwa msaada wao usioyumba.”
Katika kesi ya serikali iliyowasilishwa katika Jiji la New York Alhamisi hii, Cassie alimfungulia mashtaka Diddy kwa tuhuma za kumbaka na kumnyanyasa kimwili ikiwa ni pamoja na kumpiga ngumi, kumpiga mateke na kukanyaga akiwa juu yake wakati wa mahusiano yao huku akimuingiza kwenye uraibu wa pombe pamoha na madawa ya kulevya. P.Diddy pia alisema katika taarifa kwamba walitatua suala hilo kwa amani. “Namtakia kila la heri Cassie na familia yake.”