CEO wa Bad Boy Entertainment na business mogul Sean “Diddy” Combs maarufu kama P Diddy ni music legend, business mastermind na fashion designer. Licha ya mafanikio haya P Diddy pia anamiliki kituo chake cha Tv kiitwacho REVOLT kinacho weka headlines kubwa kama moja ya vituo vya Tv venye ushawishi mkubwa katika entertainmnet industry Marekani.
P Diddy hajaishia hapo, safari hii anakuja kivingine, na kupitia kituo chake cha Tv cha REVOLT na ushirikiano wa Pharell Williams msanii mwenye hitsong ya “Happy”, P Diddy yupo tayari kudondosha movie yake mpya iitwayo DOPE ambayo ndani yake yupo mwanae Quincy Brown na wasanii wa HipHop ASAP Rocky pamoja na Tyga.
Producers na directors wakubwa kwenye movie hii ni Pharell Williams, P Diddy na Forest Whitaker, na movie hii inaanza kuonyeshwa rasmi katika cinemas za Marekani leo.
Hapa nimekusogezea vipande vya trailer ya movie hio, unaweza kuzitazama hapa chini mtu wangu.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.