Wakati Rais John Pombe Magufuli akiwania nafasi ya kuiongoza Tanzania aliahidi kutoa shilingi milioni hamsini kwa kila kijiji ambapo leo Mei 10 2016 hoja imeingizwa Bungeni na Mbunge wa viti maalum Esther Mahawe ameuliza >>’Ni lini fedha hizo zitatolewa? Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya njia bora ya kutumia hizo fedha?‘
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Abdallah Possi akasimama na kujibu >>’Serikali imetenga shilingi bilioni 59.5 katika bajeti ya mwaka 2016/2017 chini ya fungu 21 kwa ajili ya kuwezesha wananchi vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa‘
‘Fedha hizo zitatolewa baada ya kuidhinishwa na Bunge na baada ya kukamilisha taratibu zinazolenga kuhakikisha uwepo wa tija katika matumizi ya fedha hizo‘
‘Ili kuhakikisha matumizi bora ya fedha hizo Serikali imeendelea kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji fedha hizo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya ujasiriamali‘
ULIIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA TANZANIA MAY 10 2016 KUTOKA AYOTV?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE