AyoTV

“Matatizo yaliyo kwenye uwezo wa Kiongozi na hakuyatatua, nalala mbele na huyo Kiongozi” – JPM

on

Rais Magufuli leo July 24, 2017 ameweka jiwe la msingi katika miradi mikubwa miwili; mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Tabora, Igunga na Nzega pamoja na mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Tabora na kufungua barabara mbili za Tabora – Nyahua na Tabora – Puge – Nzega.

>>>”Niwaombe viongozi Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi musimamie kero za Wananchi. Muwe mnakaa angalau kwa kila wiki kila kiongozi katika mahali alipo wasimamie matatizo ya Wananchi.

“Matatizo ya Wananchi ni mengi wanashindwa kuvumilia wanaona Rais pekee ndiye  anaweza akatatua yale matatizo. Niwaombe sana kuanzia Mkuu wa Mkoa, Mawaziri, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi muwe mnashughulikia matatizo na kuyamaliza.

“Nitakuwa natembelea mikoani nitakapokuwa napewa matatizo na matatizo hayo yawe yalikuwa chini ya uwezo wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Katibu Tarafa, Mwenyekiti wa Kijiji kuyatatua na hakutatua, mimi nalala mbele na huyo kiongozi.” – Rais Magufuli.

Kufahamu zaidi alichokisema JPM bonyeza playa hapa chini kutazama.

“Wapo waliomwita Kafulila Tumbili, Mimi nakwambia hongera” – Rais Magufuli

VIDEO: Ulipitwa na kitu Zitto Kabwe ameongea mbele ya Rais Magufuli Kigoma? Bonyeza play kutazama hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments