Mix

Kiwanda cha Tanganyika packers kurudi?, majibu yako hapa…

on

.

.

Inawezekana ulikuwa na maswali mengi kuhusu shughuli za viwanda nchini kikiwemo kile cha Tanganyika Packers sasa basi leo tumempata majibu kwa Katibu mkuu wa wizara ya Viwanda na Bishara, Uledi Mussa.

Katibu huyo akizungumza na ripota wa millardayo.com alisema..’Jana nilikuwa na kikao na katibu mkuu kiongozi  sasa  tunataka kujenga viwanda vya nyama vikubwa vya kisasa kimoja kitajengwa Dodoma, kingine kitajengwa Kibaha, kingine kitajengwa  Mbeya hivyo viwanda vitakuwa vya utaalamu wa hali ya juu kwa hiyo pale Tanganyika  Packers huwezi kuweka huduma  ya machinjio ya  nyama pale kwani tuna mpango wa kufanya kitu kingine pale‘ – Uledi Mussa

Kwa hiyo kwa maana ya sekta sasa ina maana saa hivi  tunazungumzia viwanda kwa sekta zote kwa upande wa mifungo tunasema tutakuwa na viwanda vya kisasa vya nyama, kwa upande wa Samaki hivyo hivyo na kwa upande wa misitu lazima tuache kuuza magogo tuanze kuuza mbao tuuze furniture ambazo ni za kisasa sasa maana yake huo mpango wa miaka mitano ujao ambao utatilia maanani  viwanda ni lazima tutawekeza nguvu zote tutajichimbia kwenye viwanda tuone tunaibukaje‘- Uledi Mussa

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

 

Tupia Comments