Michezo

Manny Pacquiao kurejea ulingoni mwakani, atapigana na nani? jibu lipo hapa…

on

Bondia wa kimataifa wa Filipino Manny Pacquiao ambaye mwezi May mwaka 2015 alipigana na bondia mwenye rekodi ya kutopigwa Floyd Mayweather, ameanza kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji katika bega la kulia. Manny Pacquiao mara ya mwisho kuingia ulingoni ilikuwa dhidi ya Floyd Mayweather na kushindwa kwa point.

2CE3279F00000578-0-image-a-40_1443517091461

Manny Pacquiao baada ya kushindwa pambano hilo alitoa sababu kuwa moja kati ya vitu vilivyochangia kupoteza pambano hilo ni bega lake ambalo lilikuwa na mauvu, hivyo alipaswa kufanyiwa upasuaji ila ilimlazimu kuingia ulingoni baada ya maandalizi ya pambano hilo, yalikuwa yamekamilika kwa kiwango kikubwa hivyo ilikuwa ngumu kuhairisha.

2CE3279300000578-0-image-a-39_1443517088399

Stori zilizoandikwa September 29 ni kuwa bondia huyo atarudi ulingoni mwakani dhidi ya Amir Khan, taarifa hizi zinakuja baada ya Manny Pacquiao kufanyiwa kipimo cha MRI Scan na kugundulika kuwa anaendelea vizuri. Promota wa bondia huyo Bob Arum alithibitisha wiki iliopita kuwa yupo katika mazungumzo na timu ya Amir Khan na mambo yanaenda vizuri.

2CE0076E00000578-0-image-a-37_1443517077500

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments