AyoTV

VIDEO: Msichana Mtanzania aliyeshinda Dollar 500 kupitia Facebook

on

Story kubwa kutoka Mwanza leo June 14, 2017 ni kuhusu msichana Paulina Robert mwenye umri wa miaka 18 aliyeshinda Dollar 500 za Marekani baada ya kuandika wazo kuhusu Afya ya Uzazi kupitia Facebook.

Baada ya kushinda shindano hilo ambalo liliandaliwa na Shirikala Reach for Change Africa mwaka 2016 amewafikia zaidi ya wasichana 800 akiwatembelea mashuleni kuwaelimisha namna ya kujihifadhi.

Paulina Robert amekaa kwenye EXCLUSIVE ya Ayo TV na millardayo.com na kueleza namna alivyoshinda kiasi hicho cha fedha na alivyozitumia.

>>>”Shindano hilo lilikuwa linahusisha watu mbalimbali kutoka Bara letu la Afrika. Ilikuwa haijalishi umri – umri wowote, jinsia yoyote, eneo lolote lile ambalo unaishi ilimradi unaishi Afrika. Lilikuwa linahusu kwamba endapo wewe kama mtu yeyote tu ukipewa Dollar 500 za Marekani, utafanya nini kwenye Jamii yako kuhusiana na watoto?”Paulina Robert.

ULIPITWA?? Kauli ya Tundu Lissu kuhusu madini akisema: “Mungu anasikia…mtaniambia.” Baada ya JPM kukabidhiwa Ripoti ya Pili ya Makinikia.

 

Soma na hizi

Tupia Comments