Mkuu wa wilaya ya pangani Zainab Abdallah amesema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kupeleka umeme kwenya kila kijiji na kumaliza kilio cha mda mrefu ambacho kilikuwa kuikiwakabilia wananchi wa wolla hiyo.
Akizungumza katika ziara ta Mwenyekiti wa CCM mkoa watanga Abdulhaman Abdalah wakiti akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya alisema kazi hiyo imefanyika katika kipindi cha mikama miwili baada ya serikali kutoa shilingi shilingi milioni mianne zinazotokana na mradi wa REA.
“Mhe Mwenyekiti kwa kweli pangani imetekeleza ila ya chama kwa asilimia kubwa kwenye maswala mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya umeme hapa pangani ndio wilaya ya kwanza Tanzania kwa Vijiji vyake vyote kuwa na umeme
Mkuu wa wilaya Zainab alisema Pangani ya sasa si ile aliyoikuta miaka ya nyuma na akawataka wananchi wamuunge mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya nchini.
“Ndugu zangu tuhakikishe tunamsaidia Mwenyekiti wetu ili CCM mkoa wa Tanga iweze kushinda uchaguzi wa serikali ya mitaa mwakani. Sisi Pangani tutaongoza hakuna hata kitongoji kimoja kitakachokwenda upinzani lakini pia tutaongoza kwa kura mwaka 2025 kwa kumpa Rais wetu,” alisema.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajab alisema tangu Waziri Awesso awe mbunge katika jimbo hilo amefanya mambo makubwa katika sekta za elimu, afya, maji na miundombinu.
“Ndugu zangu watu wasiwadanganye barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Tanga-Pangani-Makurunge hadi Bagamoyo ina mkono wa Waziri huyo kwa kuwa alikuwa akiipigia kelele bungeni.