Papa Francissiku ya Jumataano ameripotiwa kuugua nimonia katika mapafu yote mawili hali mbaya zaidi kwa papa huyo mwenye umri wa miaka 88 ambayo ilizua wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kupambana na maambukizi kulingana na Vatikani .
Katika Update mapema Jumatano asubuhi, msemaji wa Vatican alisema Francis alitumia usiku wake wa tano katika hospitali ya Gemelli ya Roma kwa amani. “Alikuwa na usiku mtulivu, aliamka na kupata kifungua kinywa,” alisema.
Vatikani siku ya Jumanne ilithibitisha anaugua pneumonia na kusema amepata maambukizi kaika mfumo wa upumuaji ambayo inahitaji matumizi ya matibabu ya cortisone antibiotics.
“Vipimo vya maabara, X-ray ya kifua, na hali ya kliniki ya Baba Mtakatifu inaendelea kutoa picha tata,” Vatican ilisema.
Hata hivyo papa, ambaye sehemu ya juu ya pafu lake la kulia iliondolewa akiwa kijana, yuko katika hali nzuri na anashukuru kwa maombi ya kupona kwake, Bruni alisema katika chapisho la awali