Top Stories

Papa Benedict wa 16 ana hali mbaya

on

Gazeti la Passauer Neue Presse la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Papa Benedict mwenye umri wa miaka 93 anasumbuliwa na ugonjwa unaotokana na kirusi kinachosababisha pelepele usoni na maumivu makali, kwa mujibu wa mwandishi wa tawasifu ya Papa huyo, Peter Seewald.

Kwa mujibu wa Seewald, “Papa kwa sasa ana hali dhaifu sana, limeandika gazeti hilo, akili na uwezo wake wa kufikiri bado viko makini lakini sauti yake inasikika kwa shida sana.”

Emeritus Pope Benedict XVI is pushed in to a bus in a wheelchair, in Regensburg, Germany, Thursday, June 18, 2020. The Vatican says Emeritus Pope Benedict is in Germany to be with his brother, who is in poor health. Benedict on Thursday arrived in Regensburg, Germany, where his brother, the Rev. Georg Ratzinger, lives, and where “he will spend the necessary time,” the Vatican said in a statement. (Daniel Karmann/dpa via AP)

Seewald alimtembelea Papa Benedict Mjini Rome siku ya Jumamosi kumkabidhi tawasifu yake.

Kwenye mkutano huo licha ya kuumwa kwake, Papa alikuwa na matumaini na akasema kwamba endapo hali yake itaimarika, atachukuwa kalamu tena aandike,” 

RAIS MAGUFULI APIGA SIMU, AONGEA NA SHILOLE “MNA SURA NZURI MMETISHA”

 

Soma na hizi

Tupia Comments