Shirika la afya duniani WHO mwezi huu lilitangaza ugonjwa wa homa ya nyani uliosambaa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na baadhi ya mataifa ya Afrika kuwa dharura ya afya ya umma kimataifa.
WHO imehimiza kutengenezwa na kusambazwa kwa chanjo zaidi dhidi ya ugonjwa huo.
Mpox imeenea zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imesababisha vifo vya zaidi ya watu 570 mwaka huu. Mlipuko wa ugonjwa huo pia umeripotiwa nchini Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda na mgonjwa wa kwanza wa mpox aliripotiwa nchini Sweden wiki iliyopita.