Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amerejea kazini baada kupumzika kwa siku moja kutokana na changamoto za homa, imethibitisha ofisi ya Vatican.
Siku ya Ijumaa msemaji wa Vatican Matteo Bruni alisema kuwa raia huyo wa Argentina hangeweza kukutana na watu kama alivyokuwa amepangiwa “kutokana na hali ya homa”.
Haikuwa wazi ni nani papa huyo alitarajiwa kukutana naye, kwani ajenda yake ya siku haikuwekwa wazi.
Katibu wa mambo ya nje wa Vatican Pietro Parolin alisema kiongozi huyo mwenye umri mkubwa huenda amechoka kutokana na mipango mingi kwenye ratiba yake.
Papa Francis alikuwa na mikutano minane Alhamisi, kulingana na ratiba yake iliyochapishwa. Siku ya Jumatatu, amepangwa kukutana na rais wa Italia Sergio Mattarella.

Papa mwenye umri wa miaka 86, alilazwa hosipitalini kutokana na matatizo ya kupumua miezi miwili iliyopita, amepangiwa mambo mengi kwenye ratiba yake ya kikazi.