Top Stories

Papa Msofe afikishwa Mahakamani kwa utakatishaji Milioni 900

on

Mfanyabiashara maarufu Marijan Msofe maarufu ‘Papaa Msofe’ na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo utakatishaji wa fedha wa zaidi ya TSh.Mil 900.

Si mara ya kwanza kwa Papaa Msofe kufikishwa Mahakamani hapo kwani aliwahi kukabiliwa na kesi ya Mauaji mwaka 2012 kisha alifunguliwa kesi ya Kughushi mwaka 2015.

Mbali na Msofe, washitakiwa wengine ni Wakili wa Kujitegemea, Mwesigwa Mhingo,Fadhil Mganga, Wencelaus Mtui na Joseph Haule na miongoni mwa mashitaka yanayowakabili ni Kuratibu Genge la uhalifu,utakatishaji fedha na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi, hivyo haina dhamana ambapo shauri hilo limehairishwa hadi December 16, 2019.

KIKONGWE ALIEJIFANYA HAJUI KISWAHILI AWAVUNJA MBAVU WATU AKIDAI SHAMBA LAKE KWA WAZIRI

Soma na hizi

Tupia Comments