Michezo

Alichokisema Papa Niang kipo hapa kuhusu Simba na Yanga pia (+Audio)

on

August 21 mshambuliaji kutoka Senegal Papa Niang aliwasili katika klabu ya Simba akitokea kwao Senegal, Papa anawasili Simba ikiwa ni siku ya pili toka utangazwe ujio wake katika klabu ya Simba, kama kawaida timu ya millardayo.com pamoja na kuwa na uchovu kutokana na safari ndefu alitoa dakika kadhaa kufanya exclusive interview na millardayo.com.

IMG-20150821-WA0048[1]

Team ya millardayo.com ilitaka kufahamu vitu kadhaa kutoka kwa mchezaji huyo wengi tunafahamu kuwa ukiwa na ndugu aliye katika nafasi fulani ni rahisi kukuvuta na wewe ukawa juu au kukuonyesha njia za kupita vipi kwa Papa Niang ambaye ni ndugu wa damu wa mchezaji wa zamani wa Senegal na klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa Mamadou Niang  aliwahai kumfanyia mipango mdogo wake ya kucheza Ulaya?

IMG-20150821-WA0045[1]

“Nilipo zungumza wa wakala wangu aliniambia kuhusu Simba na Yanga, nimewahi kuingalia Yanga katika mitandao ni kaona kuwa ni bingwa wa msimu uliopita, nimecheza Ulaya kwa miaka minane, kabla ya kusajiliwa Aubameyang mimi nilikuwa mchezaji niliyependekezwa kusajiliwa sema klabu yangu ilihitaji dau kubwa”>>>Papa Niang

IMG-20150821-WA0033[1]

Mamadou Niang amewahi kumfanyia mpango mdogo wake wa kucheza Ufaransa kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na winga kutokea Gabon ambaye pia anaichezea klabu ya Borusia Dortmund ya Ujerumani kwa sasa Pierre-Emerick Aubameyang, Papa Niang alishindwa kucheza Ufaransa baada ya klabu iliyokuwa ina mmiliki kutoka Finland kutaka dau kubwa huku kwa upande wa Aubameyang alikuwa mchezaji huru.

Pierre-Emerick-Aubameyang

Huyu ni Pierre-Emerick Aubameyang aliyekuwa mbadala wake baada ya kushindwa kuuzwa kwenda Ufaransa

Hii ni sehemu ya Interview ya Papa Niang na millardayo.com

<

p style=”text-align: justify;”>PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments