Magazeti

Kama hujakutana na kurasa za MAGAZETI ya TZ leo, karibu uzisome hizi stori kubwa TANO..

on

Too BusyJAMBO LEO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum DAR limesema wafuasi wa Askofu Gwajima ni marufuku kutia mguu eneo atakalohojiwa Askofu huyo, ambapo kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Askofu huyo kuwataka wafuasi hao kumsindikiza kuelekea kituoni hapo.

Napenda kutumia nafasi hii kumuomba GWAJIMA awaambie wafuasi wake hawahitajiki kufika eneo hilo.. anayehitajika ni yeye na Mwanasheria wake”—Kamanda Suleiman Kova.

Kamanda Kova amesema iwapo kila mtu atafuata taratibu hakuna nguvu itakayotumika.

TANZANIA DAIMA

Vitendo vya wafanyabiashara kupigwa na kunyang’anywa mali zao kwa kisingizio cha kusafisha Jiji vimezidi kujitokeza ambapo ni kinyume na agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye aliwataka Wakuu wa Wilaya na Mikoa kukaa na wafanyabiashara hao kuangalia namna watakavyofanya biashara zao ili kuondoa vurugu.

Waandishi wa Gazeti la TANZANIA DAIMA walishuhudia Askari wa Jeshi la Polisi na Mgambo wakitembeza kipigo kwa wamachinga kwa madai kuwa walikuwa wakifanya biashara maeneo ambayo hayajaruhusiwa huku shuhuda mmoja akisema kwamba kashuhudia Askari hao wakiwa na bunduki wakiwavamia na kuchukua bidhaa za wamachinga hao bila kuziorodhesha kama inavyotakiwa.

Tukio lile lilikuwa halituhusu lakini kilichotukera ni kuona Askari ambaye anategemewa kuwa mlinzi wa amani ndiye anakuwa wa kwanza kuvunja amani kwa kuwapora wananchi mali zao tena kwa kutumia silaha”—alisema shuhuda huyo.

MWANANCHI
Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya kuzuia malori yanayoharibu barabara.

Yupo Waziri ambaye alisema malori makubwa yanaharibu barabara hivyo mizigo yote inatakiwa kusafirishwa kwa Reli lakini mpaka sasa hajatekeleza.. kama ningekuwa na uwezo ningemchapa makofi” alisema Askofu Evarist Chengula.

Pamoja na kwamba Askofu huyo hakutaja jina la Waziri huyo lakini aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliwahi kutamka kauli kama hiyo ambapo alipoulizwa kuhusu kilichokwambisha kauli yake amesema kwamba ile haikuwa kauli yake ila ya Serikali, hivyo wa kuulizwa kwa sasa ni Waziri husika Wizara hiyo ambaye ni Samuel Sitta.

NIPASHE

Tukio la kujiua kwa askari Polisi wa kituo cha polisi Sikonge, Tabora, PC Charles Mkoyi limechukua sura mpya baada ya ndugu kueleza utata wa majeraha aliyonayo ndugu yao na malalamiko yaliyoelezwa na marehemu siku chache kabla ya kukutwa na umauti.

Ndugu wa marehemu huyo wamedai kabla ya kifo chake alilalamika kunyanyaswa na mmoja wa viongozi wa kituo hicho tangu alipoingia kazini.

Baadhi ya malalamiko aliyotueleza ni kupangwa zamu zisizo na mpangilio, kwa mfano, anakesha kazini badala ya kupumzika anatakiwa kurudi tena kazini…muda mwingi alikuwa anachoka sana na hata alipolalamika hakuwahi kusikilizwa na kiongozi huyo.”

Alisema utata unaanza Kituo cha Polisi alichodaiwa alijipiga risasi kwa kuwa alitolewa haraka na kupelekwa Hospitali ya Mkoa, huku picha zilizopigwa kwa ajili ya kuonyeshwa familia na upelelezi, zikionyesha amekaa kwenye kiti akiwa amekumbatia silaha.

Tunavyofahamu eneo lolote lenye tukio la mauaji kama hayo, mtu haruhusiwi kufika wala kusafishwa hadi zipigwe picha na hata ndugu waone, lakini inaonekana walimnyanyua na kumkalisha kwenye kiti na kumpiga picha, kwa muda mfupi palisafishwa na mwili ukapelekwa Hospitali ya Mkoa. Tunajiuliza haraka hiyo ya nini?” alihoji ndugu huyo.

Alisema kinachozua utata zaidi ni jinsi Charles alivyojipiga risasi kwa kuwa inaonyesha risasi iliingilia nyuma na kutokea mbele ambako kulikuwa na mfumuko mkubwa na nyuma tundu dogo, jambo ambalo lina shaka kwa kuwa kwa uelewa wa kawaida anawezaje kujipiga risasi kisogoni.

Ndugu hao walidai baada ya kufika kwenye kituo hicho, walionyeshwa barua mbili zilizoandikwa na askari huyo, moja ikiwa ya kikazi na nyingine ya familia na kwamba walisomewa kiasi ya familia na ya kikazi haikusomwa na hawakupewa.

Tunajua mwili wa askari unaposafirishwa wanabeba na vitu vyake vyote, wanajua alikuwa hajaoa, hana ndugu, wameacha vitu vyake vyote, kesho tunavunja matanga ndiyo siku ya kugawana nguo za marehemu, kwa mazingira haya tutagawana nini?” alihoji ndugu huyo.

Waliongeza kuwa hakukuwa na ukaribu wa polisi katika mazishi, alikuwa askari mwenzao lakini alizikwa kama raia wa kawaida.

Alisema walionana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda na kumueleza malalamiko yote na kuahidi kuyafanyia kazi, huku akisema ndani ya Jeshi la Polisi kuna utaratibu wa kufikisha malalamiko yoyote yanayohusu askari wao.

Waambie hao ndugu waje kuniona badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari,” alisema Kamanda Kaganda.

NIPASHE

Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.

Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku kuhusika na kifo cha mtoto huyo.

Diwani wa Kata hiyo amesema alipata taarifa za mtoto huyo kuuawa na baadaye kuuawa mwanamke aliyetuhumiwa kuhusika na tukio hilo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mtendaji wa Kitongoji hicho walikamatwa na Polisi baada ya nyumba za watu wote kukimbiwa baada ya tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha tukio hilo kutokea na kusema kuna watu wawili waliokamatwa kwa ajili ya upelelezi.

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments