Hii ni sehemu ya pili ya mahojiano ya Mfanyabiashara Maarufu Tanzania, Saidi Lugumi akielezea fursa za kibiashara zilizopatikana kwa Rais wa Awamu ya Tano, historia ya urafiki wake na Mstaafu Jakaya Kikwete.
Lugumi amesema Rais Samia ni Rais ambaye ni muwazi ukishalipa kodi yeye hana shida na wewe ambapo wanazidi kuiombea Serikali yote katika kila hatua wanayoifanya.
”Huyu mama kafungua milango yote ukiona mfanyabiashara analalamika basi ana matatizo yake”
Lugumi amesema hayo alipofanya mahojiano na Millard Ayo, Jijini Dar es Salaam baada ya kufanya sherehe na watoto anao walea zaidi ya 7000 aliokula nao, kucheza pamoja na kuogelea.
Aidha amesema “mimi hawa watoto ndio marafiki zangu sina rafiki baada ya mama yangu kufariki sina tena rafiki zaidi ya hawa watoto kwa sababu marafiki wengi ni wanafki, hawa watoto watakula watasoma ata siku nikifa bado wataendelea kula na kusoma”,
katika hatua nyingine Lugumi mwenye umri wa miaka (51) amelezea namna aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Jakaya Kikwete alimfahamu tangu kipindi ajapata mafanikio .
“Ni Mtu ambaye ana moyo wa kipekee, akiwa Waziri alikuwa rafiki wa baba yangu kipindi hicho baba alikuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu ananijua kuliko watu wote wanavyonijua hapa”,