Michezo

Mfahamu Pascal Wawa wa Azam FC, kuacha shule akiwa na umri wa miaka 12 na mengine (+Audio)

on

January 18 mtu wangu wa nguvu na kukutanisha na exclusive stori ya maisha ya beki wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya Azam FC Pascal Serges Wawa, wengi tunamfahamu kwa umahiri na umakini wake wakati ambao yupo uwanjani, wengine hawamjui Pascal Wawa ametokea wapi.

Katika exclusive interview na millardayo.com Pascal Wawa alikubali kueleza ukweli wa historia ya maisha yake hadi kufikia hapo alipo, Pascal Wawa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 12 na kuamua kujikita katika soka, kitu ambacho mama yake hakupenda na hakumuelewa, kwani alikataa maamuzi ya Wawa.

DSC_0018

Wawa ambaye mke wake ana masters, anaamini kilichomfanya afanikiwe ni kabla ya baba yake hajakata roho alimwambia acheze soka atafanikiwa, kitu ambacho kilikuwa kama baraka kwake, kwani nafsi ya baba yake itamlinda na kumpa baraka zote. Wawa ametokea familia yenye watoto 11, yeye akiwa wa nane, wanawake sita na wanaume watano. Wawa hakuwahi kupewa sapoti na mtu yoyote kutoka katika familia yake ili acheze soka.

DSC_0015

“Nimetokea familia ya watoto 11, mimi nikiwa wa nane, kitu cha mwisho baba yangu kuniambia kabla hajafariki aliniambia nicheze soka nitafanikiwa na nafsi yake itanilinda, niliacha shule nikiwa na umri wa miaka 12 kitu ambacho mama yangu hakunielewa kabisa, kwani nilimwambia nacheza mpira ili nimsaidie, lilipo kuja suala la soka hakuna aliyenisapoti wala kunisaidia wakati mwingine nashinda na njaa” >>> Pascal Wawa

DSC_0030

Pascal Serges Wawa amezaliwa mwaka 1986 Bingerville Ivory Coast na amepita katika vituo vya soka kama Academie de Sol Beni, Wawa ambaye kwa sasa ni beki wa kati tegemeo wa klabu ya Azam FC, alijiunga na Azam FC mwaka 2014 akitokea klabu ya Al-Merrikh ya Sudan ambayo aliichezea kwa miaka minne.

Unaweza kumsikiliza sehemu ya interview yake hapa mtu wangu

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments