Michezo

Patrick Aussems aondoka Tanzania na kuacha ujumbe mzito kwa MO Dewji

on

Usiku wa December 3 2019 aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems aliondoka rasmi Tanzania baada ya kufutwa kazi Simba SC, Aussems akiwa Airport kabla ya kuanza safari inayomuonesha atapita Amsterderm Uholanzi, alitumia kurasa zake za instagram na twitter kuandika ujumbe mzito wa wazi kwa club, mashabiki na muwekezaji wa timu hiyo MO Dewji.

“Asante kwa wachezaji ambao tumefanya nao kazi kubwa pamoja, asante mashabiki kwa sapoti yenu isiyoweza kuelezeka kutoka ndani ya moyo wangu nawatakia kila la kheri, asante MO kwa kunileta nchi nzuri lakini kwa ajili ya kukua, Ni wazi Simba lazima iondoe waongo na wasioelimika katika bodi ambao ndio kikwanzo kikubwa kwa maendeleo ya club, kwa sasa ni muda muhimu wa mimi kufurahia kitu muhimu katika haya maisha familia na watu wa kweli kwa heri Tanzania” >>> Patrick Aussems

Kama utakuwa unakumbuka vizuri aliyekuwa kocha wa Simba SC Patrick Aussems alianza kusimamishwa kazi Simba SC kwa siku tano kwa tuhuma za kuondoka kituo chake cha kazi bila kuaga na baadae kufutwa kazi kwa makosa kadhaa likiwemo la kuondoka bila kuaga na kushindwa kufikia malengo ya club.

VIDEO: Pambano la round 10 Mwakinyo vs Tinampay

Soma na hizi

Tupia Comments