Marseille wana nia ya kutaka kumsajili Paul Pogba katika dirisha la uhamisho la Januari 2025, kwa mujibu wa RMC Sport.
Mfaransa huyo aliondoka Juventus hivi karibuni baada ya kukatisha mkataba wake, lakini anaweza kucheza soka la kulipwa kuanzia Machi na kuendelea.
Pogba binafsi pia ana nia ya kujiunga na kikosi cha Roberto de Zerbi na kucheza soka katika taifa lake tena.
Anaamini kwamba kuhamia Marseille kunaweza kuongeza nafasi yake ya kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kurejea uwanjani.
Pogba hajacheza soka la ushindani katika msimu wa 2024/25 na anajitahidi kujiweka sawa katika kipindi chake cha kusimamishwa.