Ajali

Mtoto wa Marehemu Paul Walker kapeleka Kesi ya Kifo cha baba yake Mahakamani, madai yake ni haya…

on

Marehemu Paul Walker alikuwa mmoja ya wakali ambao wamecheza movie za Fast & Furious… Kifo chake ni moja kati ya vifo vilivyoshtua na kuwaumiza watu wengi Duniani.

Jamaa alifariki kwa ajali ya gari aina ya Porsche Carrera GT ambayo ilikuwa inaendeshwa na rafiki yake, Roger Rodas na Paul mwenyewe alikuwa amekaa upande wa pili.. hiyo ilikuwa November 30 2013, California Marekani.

Herculesstreet

Hili ndio eneo ambalo Paul Walker alipata ajali.

Leo kuna story ambayo imepewa uzito sana mitandaoni, inahusu ishu ya mtoto wa kike wa Paul Walker ambaye anaitwa Meadow Rain Walker mwenye umri wa miaka 16… amefungua mashtaka kuishtaki Kampuni ya Porsche kwamba ajali iliyopelekea kifo cha baba yake miaka miwili iliyopita, ilitokana na gari kuwa na matatizo na anadai kwamba muundo wa gari hiyo haikuwa gari ya kutembelea, ila ilikuwa na muundo wa gari ya mashindano.

Kingine ambacho kiko kwenye Mashtaka hayo ni kwamba wanadai gari hiyo haikuwa na mfumo mzuri wa umeme, kwa hiyo ilikuwa ni ngumu pia kwa Paul pamoja na mshkaji wake kutoka salama baada ya kupata ajali hiyo… Uchunguzi wa Maofisa Usalama wa Los Angeles ulitoa Ripoti yao kwamba sababu ya ajali hiyo ilikuwa mwendokasi.

Paul alifariki wakati ambao walikuwa kwenye maandalizi ya Movie ya Fast & Furious 7

Paul alifariki wakati ambao walikuwa kwenye maandalizi ya Movie ya Fast & Furious 7

Kwenye Ripoti hiyo pia Wanausalama wanasema Marehemu wote wawili hawakuwa wametumia kilevi cha aina yoyote na wala hawakutumia dawa za Kulevya.

Wimbo ambao uliandaliwa kama Dedication kwa Paul Walker ni huu hapa.. Wiz Khalifa Feat. Charlie Puth– ‘See You Again

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments