Magazeti

Stori kubwa kwenye uchambuzi wa Magazeti April 27 2016…#PowerBreakfast (+Audio)

on

April 27 2016 millardayo.com imekurekodia uchambuzi wa magazeti kutoka Power Breakfast ya Clouds FM, ni uchambuzi wa Habari zote kubwa kupitia magazeti yaliyoandikwa leo Tanzania, Hizi ni baadhi ya Habari kubwa zilizoandikwa leo.

Mawaziri sita kikaangoni, Wakati hali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ikielezwa ni mbaya na haina mkakati wa kujinusuru, baadhi ya mawaziri waliowahi kuongoza wizara inayolisimamia wametupiana mpira kuhusu nani atawajibika  kwa hilo.

Bunge, PAC wavutana uchunguzi wa Lgumi, Sakata la mkataba wa Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, limechukua sura mpya baada ya hadidu rejea zilizotolewa na kamati kudumu ya Bunge  ya hesabu za Serikali (PAC) kwa kamati ndogo iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza mkataba huo kutofautiana na za Bunge

Ripoti ya CAG yamtia hasira JPM, Ripoti ya mthibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), imezidi kuibua namna upigaji ‘dili’ uliofanyika kwa fedha za Umma katika taasisi na idara nyeti, zikiwamo Bunge na Ofisi ya Rais Ikulu

Unaweza ukabonyeza Play hapa chini kusikiliza…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE 

ULIMISS MWENDESHA MASHTAKA KASEMA KILA KITU KILICHOMFANYA SIWEMA AHUKUMIWE MIAKA MIWILI JELA…

Soma na hizi

Tupia Comments