Magazeti

Uchambuzi wa Story kubwa redioni… Maswali yaliyowakimbiza Wagombea kwenye Mdahalo wa Urais, Waziri Mkuu Pinda nae kutangaza nia? (Audio)

on

CJ5491

Nimekurekodia Uchambuzi wa stori za magazetini zilizosikika leo redioni @CloudsFM.

Idadi ya waliotangaza Kugombea Urais kupitia chama cha CCM yafikia 22, yuko January Makamba, Balozi Amina Ali Salum, Bernard Membe, Makongoro Nyerere, Edward Lowassa, John Magufuli, Lazaro Nyalandu na Samuel Sitta.

Ishu nyingine ni hukohuko kwenye Uchaguzi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda yeye kutangaza nia ya Ijumaa wiki hii, Waziri Mathias Chikawe nae atatangaza nia ya kugombea Urais leo.

Magazeti yameandika pia maswali makubwa nane muhimu yaliyowakimbiza wagombea Urais katika mdahalo uliofanyika tarehe 08, Mdahalo mwingine umepangwa kufanyika tarehe 18 na 25 mwezi huu.

Stori nyingine ni kutoka Njombe ambako watu 100 watafikishwa mahakamani na tume ya uchaguzi wa Taifa kwa kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la wapigakura.

Unaweza sikiliza stori hizi za leo katika audio hii nliokurekodia hapa chini mtu wangu.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments