Magazeti

Ukosefu wa Chakula Shuleni TZ.. Alichosema JK kuhusu viongozi wa dini.. GWAJIMA kamgeukia Rais JK? #PB (sauti)

on

background-homeMengine yaliyosikika Jumatatu ya leo April 13, kupitia CloudsFM kwenye POWER BREAKFAST nimekurahisishia mtu wangu.. YOTE utayasikiliza pamoja na kuyasoma hapa.

Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Uchukuzi kufanya uchunguzi kuhusu mradi mpya wa Rugemalira, ajali ya basi na lori yaua watu 18 Morogoro, Shule mbalimbali za Serikali zimefungwa kutokana na ukosefu wa chakula.

Magazeti yana mengi leo, stori nyingine ni Rais Kikwete kuwataka viongozi wa dini wasiruhusu siasa ndani ya nyumba za ibada, Askofu Gwajima amemuomba Rais Kikwete avikemee vyombo vya dola vinavyomhoji mambo binafsi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Watanzania wanaoishi nje ya nchi hawataweza kupiga kura Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya bora TZ.

Katika uchambuzi wa Magazeti kulikuwa na mahojiano na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia ambae amezungumzia suala la Shule mbalimbali za Serikali zilizofungwa kutokana na kukosa chakula.

88.0 Clouds FM inasikika ukiwa Tabora.

Bonyeza play kusikiliza Uchambuzi wa Magazeti ya Leo.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments