Magazeti

Hiki ndio nilichorekodi Uchambuzi wa stori kubwa leo June 26 2015… #PowerBreakfast (Audio)

on

Microphone

Leo ni siku ya dawa za kulevya duniani,  Rais JK atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kupambana na dawa ya kulevya yanayofanyika Bagamoyo, watoto wawili wenye umri kati ya miaka miwili na mitano wameuawa kwa kuliwa na fisi Dodoma,  kingine kwenye stori za leo kinahusu kiongozi wa kundi la waasi la ADF kesi yake kuendelea kusikilizwa Mahakama ya Kisutu Dar.

Maalim Seif Sharrif kazuiwa kuingia Baraza la Wawakilishi Z’bar, CCM waitisha Mkutano wa dharura… Wakulima wameshauriwa kupanda pilipili ili kuzuia wanyama pori kuharibu mazao yao, kuna stori pia kwamba watu wanne ikiwemo raia watatu wa Kenya wamekamatwa kwa kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura Mkoa wa Mara.

Uchambuzi wa stori zote kubwa leo uko kwenye hii sauti hapa niliyorekodi #PowerBreakfast.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments