Hii ni nukuu ya baadhi ya stori kubwa zilizogusa vichwa vya habari vya Magazeti ya Tanzania, unaweza kuzisoma zote pamoja na kusikiliza sauti ya uchambuzi wake kutoka redioni.
Jeshi la Polisi limesema wapo wafanyakazi wa Benki wanashiriki kufanya uhalifu, limesema linawasiliana na uongozi wa benki kujiridhisha na ishu hiyo… Bodi ya mikopo HESLB yavunja rekodi ya kutoa mikopo zaidi ya bilioni 400 kwa wanafunzi elimu ya juu, CCM yaitaka CHADEMA kwamba kama ina nia ya dhati ya kupambana na ufisadi imuunge mkono Rais Magufuli.
Kuna stori pia kuhusu pato la Taifa kukua kwa 6.3%, huduma kwa wananchi zimeboreshwa… Harufu ya jipu yanukia mradi wa umeme Kinyerezi II, mpango wa ‘elimu bure’ ya Rais Magufuli waanza kwa kusuasua, wazazi wachangishwa chakula, Maalim Seif amwandikia barua Papa Francis kuomba aingilie kati mgogoro wa kisiasa Zanzibar.
Mahakama ya Kisutu yatupilia mbali ombi la zuio la uchaguzi wa Mameya Manispaa ya Kinondoni na Ilala Dar.
Uchambuzi wote uko kwenye hii sauti mtu wangu kutoka Powerbreakfast #CloudsFM
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.