Kwenye stori kubwa zilizoguswa na uchambuzi wa redioni unaweza kucheki na hizi mtu wangu.
Serikali yalifungia gazeti la ‘Mawio‘, baadhi ya walimu Bagamoyo walalamikiwa kuwa wanachat darasani badala ya kufundisha, Serikali yatangaza kuchukua hatua juu ya Benki iliyohusika na rushwa wakati wa kuchukua mkopo Uingereza… Waziri Charles Kitwanga amesema oparesheni ya kukamata wahamiaji haijalenga kuwakamata Wakenya, gari lasababisha taharuki Tabata Segerea baada ya kukutwa likiwa na kofia ya mwanajeshi ikiwa na damu.
Waziri William Lukuvi ataka kuorodheshwa kwa mashamba pori, wataalam wasema tendo la ndoa linasaidia kupunguza mshtuko wa moyo, mkataba wa mabasi ya mwendokasi uko mbioni kuvunjwa kutokana na tuhuma za ukiukwaji wa kanuni.
Watoto wazaliwa kwenye mabasi na vichakani kutokana na kituo cha afya kutokamilika Shinyanga… stori hizo na nyingine zote ziko kwenye audio yake pia hapa mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.