Magazeti

Wauza unga TZ? majibu ya DNA baba na mtoto? Maalim Seif Ikulu? Kagame na bandari TZ? Stori +Audio

on

Najua kuna watu wangu wanakosa time ya kusikiliza uchambuzi wa MAGAZETI redioni kila siku, uchambuzi huwa unagusa headlines kubwa kubwa zote kurasa za nje na ndani… leo December 22 2015 kuna hizi nilizozinasa.

Rais Magufuli aungana na Marais wastaafu kwenye mazishi ya dada yake JK, Tausi Khalfan Kikwete kijijini Msoga, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hana kinyongo na mtu yoyote baada ya uchaguzi 2015, yupo huru kushirikiana na kila mtu… kuna stori pia kuhusu Jeshi la Polisi Arusha kuwashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya ofisa usalama wa TANAPA.

Kuna habari pia kuhusu vipimo vya DNA kuonesha 49% ya kesi za watoto wanaishi na baba ambao sio baba zao halali… SUMATRA imerudisha kituo cha daladala Mwenge kuanzia Januari 2016, Waziri Charles Kitwanga atangaza kupambana na dawa za kulevya… iko pia stori kuhusu Rais Kagame kumpongeza Rais Magufuli kwa usimamizi mzuri wa bandari Dar, mlinzi wa mfalme wa Qatar akamatwa kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la twiga.

Rais Magufuli akutana na Maalim Seif jana na kumhakikishia kushirikiana nae kupata suluhu ya mgogoro uliopo visiwani Zanzibar…

Mgombea Ubunge wa Masasi Rashid Chuachua  (CCM) atangazwa mshindi wa Uchaguzi mdogo uliofanyika juzi… stori hizo na nyingine kwenye uzito wake unaweza kuzisikiliza hapa kutoka #PowerBreakfast Clouds FM.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments