Magazeti

Mipango ya Afande Sele na Ubunge.. CHADEMA, ACT nini kinaendelea? Kingine kuhusu Watz walio S. Africa.. >>#HEADLINES

on

Good Morning Best Wishes Photos - 226

Kwenye vichwa vya habari kubwa MAGAZETINI iko iliyoandikwa ‘CHADEMA, ACT jino kwa jino’, wanazidi kuchuana kwenye mikutano huku viongozi wake wakishutumiana, iko iliyoandikwa kuhusu wakazi wa Hanang’ Manyara kutangaza kumuunga mkono Wakili Duncan Mayomba akigombea Ubunge kwa kuwa amekuwa akiwatetea sana wakazi wa Wilaya hiyo kwenye masuala ya Kisheria.

Afande Sele kaandikwa nae, amesema anataka kuwa Mbunge wa tofauti na sio Ubunge wa kuvaa suti na kupokea Rushwa.

Chuo cha UDSM kimeshika nafasi ya kumi kwa ubora Afrika, Serikali imetangaza kuzifuta taasisi zaidi ya elfu kumi za kidini na NGO ambazo zimetajwa kuvunja kanuni mbalimbali ikiwemo kujihusisha na siasa.

Headline nyingine ni ishu ya NEC kutangaza kuwasili mashine mpya za BVR kwa ajili ya kuandikisha Wapigakura TZ ndani ya wiki hii, nyingine ni kuhusu Serikali kutangaza kuwarudisha TZ watu wote walio tayari kurudi kutoka Afrika Kusini,

Kuna mahojiano pia ambapo kasikika Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambaye amesema wanaanza kupitia mwenendo wa vyama vya Kijamii, vikipatikana vilivyokiuka kanuni na Sheria vitafungiwa.

Uchambuzi huu bonyeza play hapa uusikilize..

Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments