Michezo

Ujumbe wa kwanza aliopost Peter Cech baada ya kusajiliwa rasmi Arsenal

on

 Hatimaye golikipa Petr Cech ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Arsenal baada ya kocha Arsene Wenger kufanikiwa kukamilisha usajili wa malipo ya Paundi Milioni 10 na Klabu ya Chelsea.

Golikipa huyo wa Czech Republic alifaulu vipimo vya afya siku ya Ijumaa asubuhi na Leo rasmi ametambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Arsenal

Cech amesaini mkataba wa miaka minne na Arsenal, na atakuwa analipwa kiasi cha Paundi 100,000 kwa wiki, na anaweza kuanza kuonekana uwanjani kwenye Mechi kati ya Arsenal vs Chelsea katika mchezo wa ngao ya hisani.

Muda mfupi baada ya kutambulishwa na Arsenal, Cech alitumia mtandao wa Twitter kuwaandikia ujumbe maalum kwa washabiki wa Chelsea na kuwaaga.

Ujumbe alipost Kipa PETR CECH

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments