Aliyekuwa ‘mshereheshaji‘ wa mechi za mpira (cheerleader) wa timu ya mpira wa miguu ya Miami Dolphins ameifungulia kesi timu hiyo kwa madai kwamba alishambuliwa na timu hiyo kutokana na imani yake na kuwa bikira.
Binti huyo Kristan Ann Ware, 27, ameeleza kuwa jambo hilo lilianza mwaka 2016 wakati timu yake ikiwa London Uingereza wakati wamepumzika walicheza mchezo ambao ulimlazimu kuwaambia wachezaji wenzake kwamba yeye ni bikra.
Kristan anaeleza kuwa ilibidi awaambie wenzake kuwa ameamua kuishi bikra hadi pindi atakapoolewa na hii ni kwasababu ya uhusiano walionao na Mungu.
Anaeleza kuwa siku za mbeleni Mkurugenzi wa timu hiyo Dorie Grogan alimfata Kristan na kumwonya asizungumzie tena suala la yeye kuwa bikra.
Madai yake ni kwamba uongozi wa timu hiyo umekuwa haumfanyii ilivyo sawa na wachezaji wengine kutokana na imani yake pamoja na suala la yeye kuwa bikra.
Mwili wa Baba wa Naibu wa Waziri wa Ardhi, umeagwa leo Mwanza.