Top Stories

Mwanaume aenda Polisi kuuliza jinsi ya kuachana na mpenzi wake

on

Kutoka nchini Ujerumani, story kali ambayo imetokea kwenye mitandao mbalimbali ni ya mwanaume mmoja ambaye aliamua kwenda kituo cha polisi na kuomba ushauri wa jinsi anavyoweza kumuacha mpenzi wake.

Mwanaume huyo ambaye anatajwa kuwa na umri wa miaka 34 alikwenda kwenye kituo cha polisi cha Ludwigshafen na kueleza kuwa anataka kuachana na mpenzi wake lakini hajui ni kwa njia gani haswa anaweza kumuacha.

Moja kati ya polisi wanawake waliokuwa kituoni hapo alimwita pembeni na kumpa njia kadhaa ambazo anaweza kuzitumia. Hata hivyo maaskari wanasema kitu walichomshauri mwanaume huyo hakiwezi kutajwa hadharani.

“Tuko tayari kumshauri mtu lakini hatuwezi kumfanyia maamuzi, tunamsadia yeyote anayetaka msaada na tunamsikiliza kila mtu.”

“Ninawapa Mwezi mmoja BILIONI 2.3 ziwafikie Vijana na wakina Mama” -DC Hapi

 

Soma na hizi

Tupia Comments