Michezo

Pedro aanza na bao Chelsea.

on

pedrooo

Mchezaji mpya wa Chelsea Pedro Rodriguez ameanza maisha mapya ndani ya klabu yake mpya baada ya kuifungia bao moja huku akitoa pasi ya mwisho kwa bao lingine katika mchezo wa ligi kuu ya England ambao Chelsea ilishinda kwa matokeo ya 3-0.

Pedro alisajiliwa na Chelsea katikati ya wiki iliyopita alifunga moja kati ya mabao matatu ambayo yalifungwa na wachezaji raia wa Hispania ndani ya Chelsea ikiwa ni ishara ya matunda ya usajili ambao Chelsea imeufanya .

Ushindi huu dhidi ya Westbromwich Albion unakuwa ushindi wa kwanza kwa Chelsea msimu huu baada ya timu hii kuanza ligi kwa kasi ya chini ambapo walifungwa na Manchester City huku wakitoka sare kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Swansea .

Pedro Rodriguez aliifungia Chelsea kwenye mechi yake ya kwanza.

Pedro Rodriguez aliifungia Chelsea kwenye mechi yake ya kwanza.

Tupia Comments