Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Michezo

Eti hii ndio itakuwa mechi yake ya kwanza Pep Guardiola atakapojiunga na Man City

on

Kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya FC Bayern Munich akimalizia mkataba wake, kabla ya kujiunga na Man City mwishoni mwa msimu Pepe Guardiola, tayari mechi yake ya kwanza akijiunga na Man City kuna tetesi kuwa imejulikana.

Pepe Guardiola anatajwa kuwa na tetesi mechi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Man United ambayo inadaiwa kuwa kwa wakati huo itakuwa ikifundishwa na Jose Mourinho, ila itakuwa ni michuano ya maandalizi ya msimu ‘International Champions Cup’ itakayofanyika Beijing China.

Jose-Mourinho-and-Josep-Guardiola

Kutoka kushoto ni Jose Mourinho na Pep Guardiola

Hata hivyo ukweli wa kukutana au kutokukutana utajulikana wiki hii, kwa sasa mashabiki wa Man United wanaimani kuwa Louis van Gaal atafukuzwa mwishoni mwa msimu na Mourinho atajiunga nao, wakati Man City wao walithibitisha kuwa tayari walisaini mkataba na Guardiola.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments