Ad

Top Stories

Pele apewa chanjo ya corona

on

Gwiji wa soka duniani Edson Arantez do Nascrimento maarufu kama ‘Pele’ amekuwa miongoni mwa Wabrazil wa kwanza kupewa kinga ya maradhi ya Corona.

Pele nyota wa zamani wa soka Brazil ambaye pia ni mshindi wa kombe la dunia mara 3, akitwaa mwaka 1958, 1962 na 1970 mwenye rekodi nyingi nzuri za kuvutia, amekuwa akisumbuliwa na maradhi, mbalimbali tangu kustaafu kwake soka.

”Siku ya leo ni siku ambayo sitaisahau kamwe maishani, najiona mwenye bahati sana kupata kinga hii maana maradhi haya Corona bado yapo duniani na ni janga kubwa sana”, Pele 

Taifa la Brazil ni moja ya mataifa ambayo yaliathirika sana na janga la Corona tangu kuanza mwishoni mwa mwaka 2019 ambapo rekodi zilizopo zinaonesha nchi hiyo iliripotiwa kuwa maambukizi ya watu milioni 10.6 na vifo 260,000 .

MAPYA GENIUS WA HESABU APATA SHULE YA KISHUA “KURUSHWA DARASA NI KIBOKO, ANAWAZIDI DARASA LA SABA”

Soma na hizi

Tupia Comments