Michezo

Pep Guardiola kashindwa kuwa mzalendo kwa Aguero na kueleza ukweli

on

Baada ya mshambuliaji wa Man City raia wa Argentina kuandika rekodi ya kuwa mchezaji pekee EPL aliyewahi kufunga jumla ya hat-trick 12 Sergio Aguero katika ushindi wa 6-1 wa Man City dhidi ya Aston Villa, kocha wa Man City Pep Guardiola ameeleza licha ya uwezo huo wa Aguero lakini hawezi kulinganishwa na Lionel Messi.

Jibu la Guardiola lilikuja baada ya swali kuulizwa kutokana na Aguero kuandika rekodi mpya EPL, huku akiulizwa anadhani Aguero ndio mchezaji bora aliyewahi kufanya nae kazi? Guardiola alitabasamu na kujibu kuwa ni Lionel Messi.

“Bora ni Messi (Lionel) lakini Sergio ni bora miongoni mwa waliosalia, nimekuwa nikisema mara nyingi atakufa huku akiwa anaendelea kufunga magoli tu, hicho ndio kipaji chake”>>> Pep Guardiola

VIDEO: KUMLAUMU AISHI MANULA NI KUMKOSEA HESHIMA BALAMA WA YANGA

Soma na hizi

Tupia Comments