Wikiendi iliyopita klabu ya Bayern Munich ilipokea kipigo cha 3-0 kutoka kwa mahasimu wao Borrusia Dortmund katika mchezo wa ligi kuu ya Bundesliga.
Kipigo hicho kimekuwa cha pili kwa Bayern Munich msimu huu tangu mwaka 2012, lakini pia kipigo hicho kimeweka rekodi mpya mbaya kwa kocha wao Pep Guardiola.
Kipigo cha mabao 3-0 kilikuwa kipigo cha kwanza kabisa kwa kocha Pep Guardiola kuiongoza timu iliyofungwa magoli matatu bila majibu, katika maisha yake ya ukocha Guardiola hajawahi kuiongoza timu kufungwa kwa idadi hiyo ya magoli.